HAKI:
1.Kuishi katika hali ya ushirikiano na jamii kwa ujumla bila kubaguliwa.
2.Haki ya kupata matibabu na huduma nyingine za kiafya.
3.Hali ya kupata elimu bila kipingamizi chochote na elimu juu ya kazi.
4.Haki ya kuajiriwa bila kipingamizi chochote.
5.Haki ya usiri
6.Haki ya kwenda sehemu yoyote bila kizuizi
7.Haki ya kutoa mawazo kama watu wengine.
WAJIBU KWA WATU WAISHIO NA UKIMWI.
1.Kufanya juhudi za kuzuia na kueneza ukimwi kwa watu wengine.
2.Kuwataarifu wenza wao baada ya kupewa majibu ya vipimo vyao.
3.Kufuata maelekezo juu ya matibabu ya ARVs
4.Kuto ambukiza UKIMWI kwa makusudi.
YAFUTAYO YASIFANYWE NA MTU YOYOTE KATIKA JITIHADA ZA KUZUIA NA KUPAMBANA NA UKIMWI.
1.Kuambukiza ukimwi kwa makusudi
2.Kutishia kuambukiza ukimwi kwa makusudi
3.Wazazi kuwatenga watoto wao au walezi kuwatenga watoto wenye ukimwi
4.Kutangaza habari za uongo juu ya watu wenye ukimwi
5.Kulazimisha kupima ukimwi.
6.Kukataa kutoa huduma kwa watu wenye ukimwi
7. Kuchukua faida ya kuzuia ukimwi kwa manufaa ya kiuchumi kwa mtu binafsi.
8. Kutumia pesa za misaada kwa watu wenye ukimwi kwa ajili ya shughuli za mtu binafsi
9. Kutengeneza mashirika mbali mbali yasiyokuwa na mipango thabiti juu ya kuzuia na kupambana na ukimwi.
No comments:
Post a Comment