Zaidi ya watu milioni 34 wanaishi na virusi vya HIV.
Takwimu zinaonyesha kuwa kwa mwaka 2011
zaidi ya watu milioni 34 ulimwenguni wanaishi na maambukizi ya Virusi
vya ugonjwa wa Ukimwi (VVU) kati ya hao milioni 30.7 watu wazima,
milioni 16.7 wanawake na milioni 3.4 watoto wenye umri wa chini ya miaka
15.
Hayo yamesemwa jana na Mwakilishi wa
Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Kupambana na Ugonjwa wa Ukimwi
(UNAIDS) Dkt. Raul de Melo Cabral wakati akiongea na wake wa wakuu wa
nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) waliohudhuria mkutano wa kuzuia
maambukizi ya virusi vya Ugonjwa wa Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa
mtoto kwa maendeleo ya kanda unaofanyika Maputo nchini Msumbiji.
Na Anna Nkinda – Maputo
No comments:
Post a Comment