Monday, March 10, 2008

TUHESHIMU HAKI ZA BINADAMU KWA WENYE UKIMWI

UKIMWI NA UHUSIANO LIOPO KATKA KUNYANYAPAA NA UBAGUZI KWA WENYE KUISHI NA UKIMWI:

Tokea kugundulika kwa ugonjwa huu wa UKIMWI unyanyapaa na ubaguzi vimechangia katika maambukizi ya ugonjwa huu. Na kwa kiwango kikubwa vitu hivi viwili vimeongeza athari kubwa ambazo zinakuwa pamoja na ugonjwa huu. Unyanyapaa na ubaguzi vipo katika karibu kila chi zote duniani ambapo husababisha vizuizi katika jitihada za kupunguza maambukizi ya ugonjwa huu.

Unyanyapaa unapelekea ubaguzi kwa watu waishio na UKIMWI pamoja na uvunjaji wa haki za msingi za binadamu ambapo huathiri maisha ya binadamu kwa kiwango kikubwa kwa waishio na UKIMWI.

UMNYANYAPAA, UBAGUZI NA UVUNJAJI WA HAKI ZA BINADAMU:

Vitu hivi vitatu vinaouhusiano wa karibu kwa maana kwamba kufanya kimoja wapo hupelekea kutokea kingine.Kwa mfano kufanya unyanyapaa kunapelekea uvunjaji wa haki za binadamu. Kwa njia moja ama nyingine unyanyapaa unapata mizizi yake kutokana na UBAGUZI, ambapo hupelekea watu kujiingiza katika vitendo ambavyo huathiri haki za watu waishio na UKIMWI. Kwa maana hiyo ubaguzi ndio chanzo kikubwa cha UNYANYAPAA.

Kuna uhusiano mkubwa wa ukosekanaji wa kulinda na kuheshimu haki za binadamu na UKIMWI. Uvunjaji wa haki za binadamu unaweza kuongeza athari za UKIMWI, walio katika hatari zaidi na jitihada za kuzuia UKIMWI.

ATHARI, uvunjaji wa haki za binadamu na kusababisha ubaguzi unaongeza madhara ya janga hili la UKIMWI. Siamini kama mbinu pekee zitumikazo katika kupambana na janga hili hatari zinatosha kama tu HAKI ZA BINADAMU haziheshimiwi. Kwa mfano mtu aliefukuzwa kazi kwa kuwa tu kaambukizwa UKIMWI anapata matatizo mengi sana baada ya kufukuzwa kwake hii ikiwa ni pamoja na kukosa njia za kujikimu kimaisha, huduma za afya na matatizo mengi mengine ambapo mwisho wa siku mtu huyu hujikatia tama na kuamua kujiua au hata kuambukiza ukimwi kwa kakusudi.

WALIO KATKA HATARI ZAIDI, watu huwa katika hatari zaidi ya kuambukizwa pindi haki za kijamii, kiuchumi, kisiasa na kiutumaduni zinapokuwa haziheshimiki na kulindwa. Kwa mfano wanawake huwa katika hatari zaidi ya kuambukizwa UKIMWI pale wanapokuwa hawana nguvu za kisheria ya kufanya maamuzi ya maisha yao au watoto wanaposhindwa kugundua umuhimu wa elimu na haki yao ya kupata habari basi vitu hivi huongeza ongezeko la watu waliopo katika hatari zaidi. Pia kukosekana haki ya kupata huduma ya afya husababisha ongezeeko kwa watu na vikundi vingine vya walio katika hatari zaidi kwa mfano watumia madawa ya kulevya, wakimbizi, wahamiaji na hata wafungwa.

Pindi haki za binadamu zinapovunjwa, zinapokuwa haziheshimiki mfano uhuru wa kusema, au uhuru wa kushirikiana na wengine na uhuru wa kushiriki katika shughuru zingine za umma kama zilivyotajwa katika ibara ya 20 na 21 ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania ya mwaka 1977 na inayobadilishwa kwa vipindi tofautitofauti. Ni vigumu kwa asasi zisizo za kiserikali kufanya kazi zake pasipo kulinda na kuheshimu haki za binadamu.

Kwa mtazamo wangu, ukimwi utapungua pindi kutakapo kuwa na ulindaji na kuheshimu haki za binadamu. Unyanyapaa na ubaguzi pamoja na madhara yake katika haki za binadamu yataondolewa kwa kufuata utaratibu wa ulindaji wa haki za binadamu.

Pamoja na mambo mengine nitafafanua kuhusiana na ibara ya 30 ibara ndogo ya 3 ya Katiba ya Jamuhuri ya MUUNGANO ya Tanzania ya mwaka 1977 iliyobadilishwa kwa vipindi tofauti tofauti.

No comments: