Monday, August 20, 2012
WAJIBU WA KILA MTU AU TAASISI KATIKA KUPAMBANA NA UKIMWI
Sheria hii inaweka wajibu kwa kila mtu anayeishi ndani ya Tanzania Bara, kila
kitengo kinachofanya kazi ndani ya Tanzania Bara, na kila shirika lililosajiliwa ndani
ya Tanzania Bara wa kufanya yafuatayo;
-Kuuambia umma na kuuelimisha juu ya vyanzo vya ugonjwa wa UKIMWI, jinsi
maambukizi yanavyotokea, madhara yake na jinsi ya kudhibiti maambukizi
ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI.
- Kupunguza kuenea kwa virusi vya UKIMWI na UKIMWI.
- Kupunguza uwepo wa magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya ngono
zembe katika jamii.
- Kupunguza madhara yanayosababishwa na virusi vya UKIMWI na UKIMWI.
-Kulinda haki za watoto yatima kwa kufanya yafuatayo:
i. Kuwapatia huduma za afya na za kijamii;
ii. Kukataza upimaji wa virusi vya UKIMWI kwa lazima labda kama
ulazima huo ni kwa mujibu wa sheria; na
iii. Kupinga unyanyapaa na ubaguzi kwa waathirika wa Virusi wa
UKIMWI.
-Kupinga mila potofu ambazo zinachangia maambukizi ya UKIMWI na virusi
vya UKIMWI katika jamii.
- Kutetea na kuendeleza mila zote nzuri ambazo husaidia kupunguza
maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI katika jamii.
- Kuwasaidia watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI na UKIMWI kupata
ushirikiano wa kutosha kutoka katika jamii hasa kwa kuwawezesha kufikia
huduma za afya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment