Friday, January 4, 2008

SERA YA TAIFA YA KUDHIBITI UKIMWI YA MWAKA 2001

Baada ya jitihada mbali mbali za serikali katika kupambana na UKIMWI hapa nchini kwetu Tanzania iliamua kutengeneza sera ya taifa ya kudhibiti ukimwi itakayotoa maelekezo katika sekta mbalimbali za nchi yetu jinsi ya kupambana na UKIMWI.

Sera hii ya taifa ya 2001 ilikuwa na madhumuni ya pamoja katika
kupambana na kuzuia UKIMWI dhumuni kubwa la SERA hii ya UKIMWI ya mwaka 2001 ni kutoa muundo wa uongozi na kuendesha sekta mbali mbali juu ya kupambana na ukimwi.

Lakini pia SERA hii ina malengo mengine mengi miongoni mwayo ni haya yafuatayo:

1. Kuzuia kuenea kwa UKIMWI kwa kuunda na kuimarisha ufahamu wa UKIMWI kupitia uwajibikaji, mawasiliano, na kubadili tabia katika sekta zote nchini Tanzania. Pia kuzuia maambukizi mapya.
2. Sera hii ya UKIMWI ya 2001 inahimiza kupima kwa hiari.
3. Inatoa pia muongozo wa kuwa na mikakati ya kuwatunza wenye UKIMWI kupitia misaada ya kijamii, na kupinga kuhusu unyanyapaa, na pia Kuhakikisha upatikanaji wa dawa na matibabu kwa watu waishio na UKIMWI.
4. Pia sera hii inahusika na kuruhusu tafiti mbali mbali kuhusu UKIMWI na kuanzisha kupatikana kwa habari za kisayansi zitokanazo na tafiti hizi.

Ndugu zangu watanzania SERA hii ya UKIMWI ya 2001 pamoja na muhimu wake katika kupambana na UKIMWI inamapungufu makubwa ambayo naiomba wizara ya AFYA kuipitia na kuongeza vitu hivi ambavyo naamini kama tupo katika mapambano ya kweli juu ya janga hili basi tuyatilie maanani na tuyafanyie kazi ili MAPAMBANO yetu yafikie malengo.

1. SUALA LA WALEMAVU,ndugu watanzania sera hii imecha kabisa kutaja suala la walemavu na hatari juu yao ya kuambukizwa UKIMWI.Hakuna palipoonyesha katika SERA hii njia za kuwalinda walemavu kotokana na hatari ya kuambukizwa UKIMWI.Wenye ulemavu wapo katika hatari kubwa ya kuambukizwa ukimwi na hivo kunaonekana kuna hitajiokubwa la kuirekebisha SERA hii ili iwajumuishe wenye ULEMAVU.Watu hawa wanatakiwa wapewe elimu na walindwe kutokana na janga hili la ukimwi.
2. WAKIMBIZI, ndugu zangu watanzania, Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi zinazo wapokea wakimbizi toka nchi jirani mara kwa mara panapotokea machafuko nchini kwao. SERA hii pia imeshindwa kuonyesha njia zitakazo tumika kuwalinda wakimbizi hawa na hatari ya UKIMWI, lakini pia kuwalinda watanzania waishio karibu na makambi ya wakimbizi hawa.Hivyo wakimbizi hawa wanakuwa katika hatari ya kuambukizwa ukimwi lakini pia watanzania waishio karibu na makambi hayo wanakuwa hatarini pia kuambukizwa UKIMWI.

NDUGU ZANGU HUU NI MFULULIZO WA MAKALA MBALI MBALI ZA KISHERIA KUHUSU UGONJWA HUU NA HAKI ZA BINADAMU.NITAANZA KUCHAMBUA SHERIA ZOTE ZA TANZANIA ZIVUNJAZO HAKI ZA BINADAMU KWA WAGONJWA WA UKIMWI ILI TUZIJADILI KWA PAMOJA ILI KUWAWEZESHA WATUNGA SHERIA KUZIREKEBISHA ILI ZIWALINDE NA ZIWANUFAISHE WAISHIO NA UKIMWI NA SI KUWANYANYAPAA NA KUWABAGUWA.

1 comment:

Anonymous said...

Nimepata blog yako Kupitia Michuzi blog. Hongera nimeipenda na nafurahia kuona moyo huu wa kufungua blog ya awareness. Hat aikisaidia mtu mmoja ni vizuri kabisa...

one more thing ...naomba uondoe hii msg ukishapata maelekezo ...ni just for you..please.... hapo kwenye maelezo yako basi weka

I am a student.... Not I am the student... I know ni vitu vidogo vidogo lakini watu watakuchukulia serious wasipona vitu kama vivyo vya haraka haraka...Mimi nasomaga blog kutokana na credibility ya mwandishi. Blog ziko nyingi sana lakini sio zote za kupoteza muda kusoma.. Basi mdogo wangu badili hiyo hapo au easy kieleweke just say "I am a 3rd year student at the Law faculty in Mzumbe Univesity, Morogoro, Tanzania...""

I hope hutachukulia email hii vibaya Najaribu kusaidia tuu....