Monday, May 19, 2008

MAMA HUYU ALIGUNDULIKA ANA UKIMWI 1994 AKIWA MJINI BUKOBA TANZANIA.AMEKUWA AKIISHI NA VIRUSI MPAKA LEO 2008 MIAKA 14 TOKEA KUAMBUKIZWA KWAKE.ALIJITOKEZA NA KUTOA USHUHUDA MBELE YA UMATI ULIOKUWEPO MKAPA HALL MBEYA SIKU HIYO. ANA WATOTO NA WAJUKUU.MTOTO WAKE WA MWISHO YUPO KIDATO CHA NNE. MIONGONI MWA MATATIZO ALIYOELEZEA NI TATIZO KUBWA LA UNYANYAPAA NA KUTENGWA. ALIIONYA JAMII JUU YA ATHARI YA UNYANYAPAA NAKUWATENGA WENYE UKIMWI.
MWANACHUO WA CHUO CHA UHASIBU TANZANIA AKISOMA RISALA KWA NIABA YA WANAVYUO WA MKOA WA MBEYA.KUBWA ALILOLISEMA NA VIJANA TUPINGE UNYANYAPAA KWA WAISHIO NA UKIMWI

WAKATI WA UWASHAJI MISHUMAA KAMA ISHARA YA KUWAKUMBUKA WALIOKUFA KWA UKIMWI INAANZISHWA NA BAROZI WA UINGERAZA NCHINI TANZANIA.
KILIKUWA KIPINDI KIGUMU NDANI YA UKUMBI HUU MAANA NDIPO MACHOZI YA WATU WENGI YALIANZA KUTOKA KWA HISIA ZILIZO KUWEPO NDANI HUMO MWA UKUMBI HUO.
UKIMWI NI WETU SOTE,WANAO ISHI NA UKIMWI NI NDUGU ZETU,TUSIWANYAPAE NA WALA TUSIWATENGE.

No comments: