Monday, August 20, 2012

HAKI ZA WAISHIO NA UKIMWI

HAKI ni suala muhimu kwa kila mwanadamu, kwani hutumika kukulinda kisheria.Katika miaka ya nyuma hali ilikuwa ni mbaya kutokana na suala la Ukimwi na VVU kuwa ni suala geni sana machoni na masikioni mwa jamii, hususani linapojitokeza suala la kutanabaishwa jinsi ugonjwa huo ulivyo kuanzia sababu za kuupata, dalili hadi njia za kuuzuia au matibabu.
1.  Haki ya kutobaguliwa.Kubaguliwa ni haki muhimu ambayo huweza kusababisha madhara kama ya kufikia hatua ya mhusika kuchukua hatua mbaya iwapo atakuwa akibaguliwa na jamii inayomzunguka.
2. Haki ya kupata taarifa sahihi,Kwa kiasi kikubwa hili ni tatizo lililopo ndani ya jamii kiujumla sio tu kwa wale waishio na VVU na Ukimwi tu bali hata kwa wale wenye matatizo ya aina nyingine.
Mara nyingi tumeweza kuona makosa mbalimbali ambayo baadhi ya wataalamu kama vile madaktari walivyokosea na kutoa taarifa zisizo sahihi hali iliyosababisha labda kifo au hata madhara makubwa kwa ndugu jamaa na marafiki zetu.
Kwa maana hiyo jambo muhimu ni kufahamu kuwa haki ya kupata taarifa sahihi iwapo kama ni majibu ya tatizo alilonalo baada ya kupima, kuwa hiyo ni haki yake ya kimsingi ambayo inatakiwa kutekelezwa kwa makini sana ili taarifa zake zisije potoshwa na baadae kusababisha madhara.


No comments: