Wednesday, May 21, 2008

UNYANYAPAA NA KUTENGWA KWA WENYE UKIMWI

UNYANYAPAA NA KUTENGWA KWA WENYE UKIMWI

Kunyanyapaa na kutenga imegundulika kuwa ni suala la dunia nzima linatokea kila sehemu duniani kote.Unyanyapaa unaongezeka na kuwa suala nyeti sana katika ugumu wa kusema juu ya UKIMWI.Hata hivyo kwa mtazamo wangu finyu naona kuzungumzia unyanyapaa na kutengwa kwa waishio na ukimwi ni njia moja wapo ya kupambana na kupunguza madhara ya UKIMWI.

Katika kuona umuhimu wa kuzuia unyanyapaa na kutengwa, kampeni za dunia za mwaka 2002-2003 zililenga kuondoa unyanyapaa, kutenga, na haki za binadamu. Madhumuni makubwa ya kampeni hiyo yalikuwa ni kuzuia, kupunguza na mwisho kuondoa unyanyapaa na kutenga juu ya UKIMWI unavyotokea na aina zake zote.

Unyanyaa na kutengwa kwa watu waishio na ukimwi unasababishwa na vitu vingi. Hii ni pamoja na kutoeleweka vizuri kwa ugonjwa huu, Watu wingi hasa waishio vijijini ambapo elimu ya ukimwi haifiki kwa usahihi wanaamini kuwa ukimwi unaambukizwa kwa kukutana namaanisha hata kwa kushikana mikono na mwenye ukimwi kitu ambacho si sahihi, kukosekana kwa dawa, vyombo vya habari kutowajibika vizuri juu ya kulizungumzia suala hili la ukimwi, dhana kwamba ukimwi hautibiki, pamoja na hofu nyingine za kijamii.

Madhara yake ni kwamba kumekuwepo na woga na aibu juu ya ugonjwa huu duniani pote kwa mtu mmoja mmoja na hata kwa ngazi ya serikali.Imeleta hofu na woga juu ya kuibua mijadala mbali mbali juu ya vyanzo vya ukimwi na jitihada zinazo hitajika katika ngazi zote. Pia imeleta hatari ya kuongezeka waliopo katika hatari ya kuambukizwa ukimwi. Walioambukizwa wanahisi wakosefu na ndivyo jamii inavyo wachukulia na kuwa na aibu kitu kiletacho woga, kutojiamini, na wasiwasi katika jamii. Hii inasababisha vifo vya mapema ambavyo vingine hutokana na kujiua. Haya ndiyo madhara ya unyanyapaa na kutengwa kwa watu waishio na UKIMWI.

No comments: