Monday, August 20, 2012

WAJIBU WA KILA MTU AU TAASISI KATIKA KUPAMBANA NA UKIMWI


Sheria hii inaweka wajibu kwa kila mtu anayeishi ndani ya Tanzania Bara, kila

kitengo kinachofanya kazi ndani ya Tanzania Bara, na kila shirika lililosajiliwa ndani

ya Tanzania Bara wa kufanya yafuatayo;

-Kuuambia umma na kuuelimisha juu ya vyanzo vya ugonjwa wa UKIMWI, jinsi

maambukizi yanavyotokea, madhara yake na jinsi ya kudhibiti maambukizi

ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI.

- Kupunguza kuenea kwa virusi vya UKIMWI na UKIMWI.

- Kupunguza uwepo wa magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya ngono

zembe katika jamii.

- Kupunguza madhara yanayosababishwa na virusi vya UKIMWI na UKIMWI.

-Kulinda haki za watoto yatima kwa kufanya yafuatayo:

i. Kuwapatia huduma za afya na za kijamii;

ii. Kukataza upimaji wa virusi vya UKIMWI kwa lazima labda kama

ulazima huo ni kwa mujibu wa sheria; na

iii. Kupinga unyanyapaa na ubaguzi kwa waathirika wa Virusi wa

UKIMWI.

-Kupinga mila potofu ambazo zinachangia maambukizi ya UKIMWI na virusi

vya UKIMWI katika jamii.

- Kutetea na kuendeleza mila zote nzuri ambazo husaidia kupunguza

maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI katika jamii.

- Kuwasaidia watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI na UKIMWI kupata

ushirikiano wa kutosha kutoka katika jamii hasa kwa kuwawezesha kufikia

huduma za afya.

No comments: